Naibu Katibu wa Wizara ya Kilimo Chakula na
Ushirika Bi. Sophia Kaduma wa nne Kulia, akiwa pamoja na Tume ya
Ushirikiano wa Pamoja katika sekta ya kilimo.
Akizungumza na tume kutoka pande zote mbili Tanzania na Indonesia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Mama Sophia Kaduma alisema majadiliano hayo yanalenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo pamoja na upatikanaji wa masoko. Mama Kaduma alisema ushirikiano baina ya nchi hizo mbili utahusisha katika kujenga uwezo wa wakulima, masuala ya utafiti pamoja na upatikanaji wa masoko ya mazao. Katika kujenga uwezo Mama kaduma alisema Tanzania na Indonesia itashirikiana katika mafunzo ya Muda mfupi na mrefu pamoja na kubadilishana wakufunzi ambao wataenda kufundisha vyuo mbalimbali vilivyopo katika nchi hizo. Katika mafunzo ya muda mfupi serikali ya Indonesia itafadhili masomo ya Uchumi Kilimo na kilimo cha bustani hasa katika maeneo ya utafiti, usindikaji na mbegu. Alifafanua kukuwa Indosesi itafadhili mafunzo kwa wakulima 15 chini ya mpango wa Ushirikiano wa nchi za kusini ambapo wakulima 12 watatoka Tanzania Bara na watatu watatoka Tanzania Visiwani. Aliongeza kuwa masoma hayo yataanza tarehe 1-9/07/1213 na Tanzania itagharamia nauli za washiriki wa program hiyo pamoja na pesa za kujikimu. Kwa upande wa mafunzo ya muda mrefu katika kujenga uwezo, serikali ya Indonesia itatoa ufadhili kwa watu watatu ambao watasoma shahada ya uzamili na uzamifu na mmoja ambaye atasoma masomo yalio chini ya shahada ya kwanza. Pia alisema nchi hizo mbili zitashirikana katika mambo ya utafiti wa mazao hasa katika mazao ya pamba, mpunga na viungo mbalimbali. Alifafanua kuwa utafiti huo utahusisha mambo ya GMO, majaribioa mashambani, uzalishaji wa mbegu bora, magonjwa, usindikaji na uimarishaji wa vituo vya utafiti. Mama Kaduma alisema pian nchi hizo zimekubalia kushirikiana katika katika masoko kwa kubadilishana taarifa za masoko na taratibu mbalimblia ili kuboresha biashara ya bidhaa za kilimo kati ya nchi zote mbili. Alifafaunua kuwa licha ya kushirikiana katika masoko pia Serikali ya Indonesia itashiriki katika maonesho ya kimataifa ya wafanya biashara yafanyika Dar es Salaam (Sabasaba) pamoja na maonesho ya wakulima ya Nane Nane. Ushirikianao baina ya nchi hizo mbili unalenga kuongeza tija katika kilimo, kuongeza upatikanaji wa masoko, kuongeza uzalishaji wa mazao pamoja na kukuza kipato cha mkulima. |
|||
Mazao yaliyostawi vizuri yakionyesha mojawapo ya aina ya kilimo Asili cha Mseto
Wadau wa kilimo, sera, mazingira, utawala, na mashirika ya
kimataifa, wametoa wito wa kubaini mifumo asili ya Kilimo kwa kutambua
mchango katika uhakika wa chakula na kipato.Wito huo ulitolewa katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliyojumuisha wadau hao ili kutathmini mchango wa mifumo asili ya kilimo na changamoto zilizopo ili kuiboresha na kiendeleza. Ilibainika kuwa Tanzania ina mifumo mingi ya asili ya kilimo na mifugo ambayo imedumu kwa taribani zaidi ya miaka 100 hadi 700. Katika kipindi hicho, mifumo mingi imekumbana na mabadiliko ya hali ya hewa lakini imekabili na kudumu, hii inaonyesha kuwa kuna vitu vingi vya kujifunza katika mifumo hiyo. Aidha, wadau wamependekeza mifumo ya asili ya kilimo na ufugaji kuingizwa katika sera kati ya zilizopo ili ipate nguvu ya kusimamiwa na kuendelezwa hasa ikizingatiwa umuhimu wake katika kuimarisha usalama wa chakula na kipato kwa kaya na taifa kwa ujumla. Pia wametaka mashirika ya kimataifa yaendelee kuchangia kwa rasilimali uendelezaji wa mifumo asili endelevu kwani manufaa yake ya mazingira ni ya ulimwengu. Afisa Mkuu wa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Firmat Banzi alisema kuwa mifumo asili ya kilimo ina haja ya kuendelezwa ili kuboresha na kuimarisha maarifa asili kuwezesha ushiriki wa wakulima katika utunzaji wa mifumo hiyo. Alifafanua kuwa uendelezaji wa mifumo hiyo utawapa fursa wakulima kuweza kushiriki kikamilifu katika kilimo wakiwa na uhakika wa kupata mazao mengi kuweza kujitosheleza kwa chakula na kujiongezea kipato pamoja na kuboresha hifadhi ya mazingira hasa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Washiriki kwa pamoja wamepitisha azimio linalotambua mchango wa mifumo ya asili ya kilimo na ufugaji na wametoa wito wa kubaini mifumo asili iliyopo nchini, kutathmini mchango wake na changamoto kwa lengo la kuiboresha na kuiendeleza. |
Wizara Kushirikiana na Indonesia Kukuza Kilimo
Labels:
KILIMO