HABARI MBALIMBALI ZA WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA KUTOKA BUNGENI DODOMA
KILIMO KUTUMIA SHS. 328,134,60
Habariz zote za Bunge na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.
|
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika inatarajia kutumia jumla ya shilingi 328,134,608,000/- katika mwaka ujao wa fedha.
Takwimu
hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza wakati akiwasilisha Bungeni
Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2013/14.
Alisema
kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 247,094,320,000 ni kwa ajili ya
Matumizi ya kawaida na Shilingi 81,040,288,000 ni kwa ajili ya Matumizi
ya maendeleo.
Chiza aliongeza kuwa Shilingi 210,175,943,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengine (OC) kwa ajili ya Wizara hiyo .
Aidha
,shilingi 25,602,969,000 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Wizara na
Shilingi11,315,408,000 ni Mishahara (PE) ya Bodi na Taasisi zote
zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Kwa
upande shughuli za maendeleo, Chiza alisema kuwa Wizara hiyo imetenga
kiasi cha shilingi 23,927,000,000 ikiwa ni fedha za ndani na
shilingi 57,113, 288,000 ni fedha za Nje.
Wabunge
wanatarajia kujadili bajeti ya Wizara ya Kilimo , Chakula na Ushirika
kwa kipindi cha siku mbili ambapo itahitimishwa kesho.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe. Chiza amesema
Serikali inatarajia kufufua Kituo cha Kilimo Anga ili kukiwezesha kuwa
na ndege na Wataalam watakaosaidia kudhibiti milipuko ya visumbufu vya
mazao hasa Nzige.
Mhe.
Chiza amesema kwa kiasi kikubwa Serikali imekuwa ikitegemea huduma ya
ndege kukodi kutoka kwenye mashirika ya kikanda ya kudhibiti nzige
wekundu na nzige wa jangwani ambazo wakati mwingine hazipatikani wakati
zinazohitajika.
Kufuatia
hali hiyo amesema Wizara katika mwaka wa fedha 2012/13 imekamilisha
viwango vya kiufundi (Technical Specifications) kwa ajili ya kutangaza
zabuni ya ununuzi wa ndege moja ya kunyunyuzia viuatilifu.