Serikali yazidiwa nguvu kodi ya simu
kwa ufupi
- Hata hivyo, alisema uamuzi wa kuanzisha tozo hiyo haukuwa wa Serikali bali ulipitishwa na kukubaliwa baada ya kujadiliana na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema
kwamba Serikali inapokea maoni ya wadau mbalimbali ili kuona namna ya
kufanya marekebisho ya tozo hiyo. Hata hivyo, alisema uamuzi wa
kuanzisha tozo hiyo haukuwa wa Serikali bali ulipitishwa na kukubaliwa
baada ya kujadiliana na Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa
Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
“Hayo yalipendekezwa na Kamati ya Bunge siyo
Serikali. Tena walipendekeza vyanzo 67 vya kodi likiwamo hilo la kadi za
simu. Walipendekeza tukate Sh1,450 kwa mwezi, lakini sisi Serikali
tukashusha hadi Sh1,000 yaani kila mwananchi akatwe Sh33.3 kwa siku na
mapato yatakayopatikana yatakwenda kuboresha miradi ya maji, umeme
vijijini na barabara,” alisema Dk Mgimwa.
Upinzani mkali
Wabunge wa Chadema, John Mnyika wa (Ubungo) na
Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), wamekuwa mstari wa mbele kupinga kodi
kwa kuonyesha jinsi itakavyowanyanyasa wananchi.
Mnyika amekuwa akikusanya saini za wananchi
wanaopinga mpango huo wa Serikali ili awasilishe bungeni hoja ya
wananchi kupinga tozo hiyo. Hadi sasa ameshakusanya saini zaidi ya
26,000.
Kwa upande wake, Zitto alisema kodi hiyo
haikujadiliwa kabisa kwa kuwa iliondolewa katika mapendekezo ya mapato
lakini ikarejeshwa kupitia Muswada wa Fedha ambao hutafsiri hotuba ya
Bajeti kisheria.
“Kama kodi hii haikuwa kwenye hutuba,
haikujadiliwa na Bunge, msingi wa Muswada wa Fedha kuwa na kodi hii
haupo. Kodi hii ilirejeshwa kinyemela bungeni na kupitishwa bila
mjadala.”
asante kwa kutembelea blog yetu
asante kwa kutembelea blog yetu