Kundi lisilo na fursa ya elimu
kwa kubakwa, kulawitiwa ndiyo maisha -2
Ombaomba wakiwa na watoto wao
katika eleo la Mnazi mmoja jijini Dar
es Salaam
Kwa
ufupi
Utafiti wa Shirika
la Mkombozi mwaka 2005, unataja sababu za watoto wa mitaani kuongezeka kuwa
ni wakinababa kutelekeza familia.
- *Ndoa nyingi kuvunjika na familia kuongozwa na mzazi mmoja.
- *Kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa nje ya ndoa.
- *Watu kuzaa watoto wengi wasioweza kuwalea
Wanakuja usiku kwenye
maeneo tunayolala wanatafuta wanayemtaka ili akawafanye, ukimaliza wanakupa
hela na wengine wanakunyima wanakufukuza
Juma lililopita tuliona jinsi
watoto waishio mitaani wanavyokosa fursa ya elimu na kuambulia mateso ikiwa
pamoja na kulala nje, kulawitiwa, kubakwa na kukosa mahitaji muhimu kama chakula na mavazi.
Wiki hii, watoto hao
wanaendelea simulizi la madhila mbalimbali yanayowakuta katika mazingira hayo
magumu, huku Serikali ikiainisha mikakati ya kukabilina na hali hiyo.
Watoto kulawitiwa
Mwananchi iliwahi kufanya
uchunguzi juu ya maisha ya vijana hao na kubaini kuwa, wengi hulazimishwa
kulawitiwa ama kulawiti.
“Wanakuja usiku kwenye
maeneo tunayolala wanatafuta wanayemtaka ili akawafanye, wakimaliza wanakupa
hela na wengine wanakunyima wanakufukuza,” anasema mmoja wa watoto hao.
Watoto hawa, licha ya
matatizo wanayokutana nayo, wakati mwingine huonekana kama
wasiostahili kuonekana machoni mwa baadhi ya watu, hasa viongozi wa kitaifa.
Mtoto mwingine akieleza
masaibu yake huku akibubujikwa na machozi anasema siku ya nne tangu
aingie Dar es Salaam akitokea kwao, Dodoma alikuwa amelala kwenye
kibaraza cha jengo la Soko la Kariakoo, alianza kusikia maumivu makali
sehemu za haja kubwa, aliposhtuka alijikuta katika mikono na mwanamume
aliyemwita mzee ambaye alikuwa akimlawiti.
“Nilitaka kupiga
kelele, lakini alikuwa ameniziba mdomo na amenielekeza sehemu ya ukutani,
alikuwa amechukua maboksi mengi akawa ameyaweka yametufunika kabisa, haikuwa rahisi
kwa mtu kuona kilichokuwa kikifanyika. Kwa hiyo nikashindwa kumfanya chochote,
alipomaliza akaniambia nikipiga kelele ataniua,” anaeleza na kuongeza:
“Baada ya kunifanya
vile sikuweza kulala tena siku ile, kama baada
ya wiki kupita, yule mzee alikuja tena na kunikamata kwa nguvu na kuniingiliia
tena nikiwa tena nimelala.Sasa ikawa ndiyo tabia yake mpaka ikabidi mimi nihame
lile eneo nikaja huku Uhindini.”
Mbali na mzee huyo, mtoto
huyo anasema pia kwa nyakati tofauti amewahi kukamatwa na vijana wenzake
wanaoishi mitaani ambao ni wakubwa na wakamlawiti.
Watoto wengine wanasema
kwamba, baadhi ya watu hufika kwenye maeneo wanapoishi na kusema wanataka
kuwapeleka shule, kinyume na wanavyosema huwachukua na kwenda kuwalazimisha
kufanya