Meya CCM akalia kuti kavu Arusha
Na Protas Charle Youth for Change
- Chadema waanza mkakati wa kumng’oa madarakani, Mbowe ajisalimisha polisi
- CCM yasema wanajidanganya, wanapaswa kufanya kazi na meya wa sasa
Ushindi huo unakihakikishia wingi wa wajumbe
katika baraza hilo la madiwani hivyo kuwa na fursa kumwondoa madarakani
Meya Lyimo. Doita aliahidi kuwa chama hicho kitakaa leo kutoa msimamo
kuhusu suala hilo la umeya wa Arusha.
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa CCM wa Mkoa wa
Arusha, Mary Chatanda alisema Chadema kisahau suala la kuchagua meya
mpya kwani uchaguzi wake ulishapita.
Chatanda, ambaye pia anaingia katika vikao vya
Baraza la Madiwani la Arusha kutokana na kuwa Mbunge wa Viti Maalumu,
alisema Chadema kinapaswa kufanya kazi na meya wa sasa.
“Unajua vikao hivi vinaongozwa kwa kanuni, kwa
hiyo wingi wao si hoja ya kumvua meya au kulazimisha kupitisha mambo
yao,” alisema
Mamia wafurika Manispaa
Wabunge wanne wa Chadema jana waliongoza mamia ya
wafuasi wa chama hicho katika shamrashamra ya kuwasindikiza madiwani
wanne kwenda kujitambulisha kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.
Hata hivyo, furaha yao ilizimwa na polisi baada ya kumuomba Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kuwatawanya.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU