Home » » Unafahamu kama una rafiki wa kweli au?

Unafahamu kama una rafiki wa kweli au?

Unafahamu kama una rafiki wa kweli au?




Ukikutana na mtu barabarani akakuuliza kama una rafiki wa kweli utaweza kumjibu kama ndiyo au hapana? Hapana shaka utasita kumjibu, huenda hutaweza kupata jibu moja kwa moja na kama utaweza kumjibu mara tu atakapokuuliza, utakuwa una bahati sana. Hili ni moja kati ya matatizo ya maisha. Tunapata marafiki wengi, lakini tunashindwa kuwafanya kuwa marafiki zetu wakati wote, hata wakawa marafiki wa kweli.Pengine hata sisi wenyewe tunashindwa kuonekana kama marafiki wa kweli kwa wenzetu. Lakini tujiulize Je, ni lazima tuwe na marafiki? Je tunaweza kuishi bila marafiki? Kwa hakika tunahitaji kuwa na marafiki katika maisha yetu kwa sababu ndiyo wanaotupenda na kutujali. Ni washirika wetu katika raha na shida, furaha na huzuni, tabu na raha, njaa na shibe, umaskini na utajiri, ugonjwa na afya na pengine hata katika uzima na kifo na mengineyo mengi. Husemwa kuwa na marafiki wema na wa kweli hushinda kuwa na mali.Sasa hebu turudi tulikoanzia. Acha swali la marafiki wa kweli kwa muda, ili tujiulize swali jingine. Je, ukiwaorodhesha marafiki zako wote wanaweza kufikia wangapi? Je kama ungefariki leo, unafikiri ni marafiki zako wangapi wangefika kwenye msiba wako? Kama ni wachache sana bado unahitaji kutafuta marafiki.Nina hakika kila mmoja wetu ana marafiki aliowapata katika nyakati mbalimbali za maisha. Lakini pengine kuna wengi tuliowapoteza. Pengine tumewapoteza kwa kutenganishwa na kifo. Pia wapo wale ambao tumetenganishwa nao kwa kuwa mbali, kwa kukosana au wamekata tamaa kwa kuwakatia mawasiliano . Lakini kwa liwalo lolote, tunahitaji kuwa na marafiki. Hivyo, tunapaswa kujua namna ya kujenga urafiki na namna ya kufanya urafiki wetu udumu siku zote.Kwa hakika, hakuna kitu kinachojenga urafiki kama kutendeana mema. Upendo hautupatii tu marafiki, bali hujenga heshima na utu wetu. Kwa kuwatendea watu mema na kuwa wakarimu tunapata marafiki wengi katika maisha. Tunapopata marafiki tukawapenda kwa dhati na wao wakatupenda, tukawathamini na kuwajali na wale wa kweli hatutaweza kuwapoteza.Kwa hakika, tutakuwa tumejijengea mazingira yenye matumaini ya kupata marafiki wa kweli. Tukiwa na marafiki wengi wa kweli, tutakuwa tumejipatia furaha ya kudumu katika maisha.Hebu tutafakari hiki kisa cha kweli cha marafiki:Baada ya kushambuliwa vikali kwenye uwanja wa vita, kikosi kilirejea kambini kikiwa na maiti na majeruhi wengi. Kijana mmoja alisikitika sana alipomkosa rafiki yake waliyekuwa naye kwenye uwanja wa mapambano.


Share this article :
 
Support : Swahiliclan | harold | 0752490120
Copyright © 2011. YOUTH FOR CHANGE - All Rights Reserved
Template Created by swahiliclan Published by hashork
Proudly powered by sc