Majambazi yateka mabasi mawili
IGP Sais Mwema
Kwa ufupi
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kagera, Philip Kalangi alisema majambazi wapatao kumi waliokuwa na
silaha nzito za kivita asubuhi ya Jumatatu waliteka mabasi mawili ya
abiria yaliyokuwa yakielekea katika majiji ya Arusha na Dar es Salaam.
Kagera. Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa
majambazi wameteka mabasi mawili ya abiria na kufanya uporaji katika
Pori la Hifadhi ya Biharamulo Mkoani Kagera na kupora bunduki aina ya
SMG iliyokuwa na askaRi aliyekuwa anasindikiza mabasi hayo.Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kagera, Philip Kalangi alisema majambazi wapatao kumi waliokuwa na
silaha nzito za kivita asubuhi ya Jumatatu waliteka mabasi mawili ya
abiria yaliyokuwa yakielekea katika majiji ya Arusha na Dar es Salaam.Alisema silaha zilizoonekana eneo la tukio ambazo zilitumiwa na majambazi kujihami ni SMG sita na LMG mbili.Kwa mujibu wa Kalangi, mabasi yaliyotekwa ni NBS
lililokuwa likielekea Arusha na RS lililokuwa likielekea Dar es
Salaam,ambapo kabla waliteka gari dogo na kulitumia kufunga barabara
katika hali iliyoonekana lilikuwa limeharibika.Katika tukio hilo, abiria mmoja aliyetambuliwa kwa
jina la Fredrick Rugaihura (47)mkazi wa mjini Bukoba alijeruhiwa
shingoni kwa risasi, ambapo majambazi hao walipora mali mbalimbali za
abiria zikiwemo fedha na simu.