SERIKALI: VIJANA SASA KUJIAJIRI KATIKA KILIMO CHA KIBIASHARA
Na Boniphace Nyabweta, Maelezo Dodoma.
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imekamilisha andiko la namna ya kuwavutia vijana kujiajiri katika kilimo cha biashara.
Akiwasilisha
Makadirio na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/14, Waziri
Chiza amesema kuwa andiko hilo litatumika kuandaa mipango ya kuwezesha
vijana kujiajiri katika kilimo kwa kushirikisha wadau wote.
Wakati
program hiyo inakamilishwa , tayari baadhi ya vijana wamekwishaanza
kujiajiri katika kilimo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Mhe.
Chiza amebainisha kuwa katika kijiji cha Isaka-Malilo-Igunga wahitimu
10 wa Vyuo Vikuu mbalimbali hapa nchini wamejiunga pamoja na tayari
wamepewa ekari 150 wanazozitumia kulima zao la alizeti kibiashara.
“Wizara imewezesha kwa kuwapatia chakula na pampu mbili kwa ajili ya umwagiliaji”, alisema Mhe. Chiza.
Alitaja
kikundi kingine kuwa kipo Arusha,ambacho ni cha mtandao wa wakulima
1000 cha “Home Vegetable Group” wanaozalisha mboga mboga na mahindi
machanga .
Aidha,Waziri
Chiza amebainisha kuwa katika mkoa wa Singida, kikundi cha Vijana
kimewezeshwa kulima alizeti kibiashara ambapo wamepatiwa eneo la hekta
200 kwa ajili ya shughuli hizo na mkoani Kigoma wilayani Kibondo kikundi
cha vijana wanaolima muhogo kibiashara wamewezeshwa.
Waziri
amesema, Wizara yake kupitia DASIP imetoa mafunzo ya kilimo na ufugaji
bora kwa vijana 179,698 na kuwawezesha kupata ajira katika miradi ya
jamii, teknolojia za kilimo na mifugo na kuanzisha mashamba na ufugaji.
“Kati
ya vijana hao 1,669 wameajiriwa kwenye miradi ya jamii, 1,043 katika
miradi ya teknolojia ya kilimo na 178,986 wameanzisha mashamba ya kilimo
na ufugaji bora”. Mhe. Chiza alisema.
BONIPHACE NYABWETA NI MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA
BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA KILIMO, TEKNOLOJIA NA BURUDANI
ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE
KUFIKA TULIPOKUSUDIA