Home » » Jimbo la Nzega lakosa kigezo kugawanywa

Jimbo la Nzega lakosa kigezo kugawanywa

Jimbo la Nzega lakosa kigezo kugawanywa

Share bookmark Print Email Rating

SHARE THIS STORYShare

   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanry amesema Jimbo la Nzega halina vigezo vinavyoweza kulifanya ligawanywe kuwa mawili.Mwanri alisema hayo  wakati akijibu swali la Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangala aliyeiambia Serikali kuwa haioni kuna umuhimu wa kuligawanya jimbo  lake kwa sasa.Mwanri alisema Tume

ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ndiyo yenye mamlaka ya kuchunguza na kuona kama jimbo lolote lina sababu ya kugawanywa.Mbunge wa Ngorongoro, Kaika Telele (CCM), aliuliza swali la nyongeza akitaka kujua kama kuna ubaguzi wa kugawanya wilaya za mijini na vijijini.Katika kufafanua zaidi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema vigezo vya kugawanya wilaya za mijini vinatofautiana na vijijini.Alitaja miongoni mwa vigezo vya kugawanya wilaya ya mjini ni pale wakazi wake wanapozidi 276,000, wakati vijijini ni pale inapozidi 206,000. Vilevile alisema kuna vigezo vingine kama vile uchumi wa eneo husika, kipato na mtandao.wa mawasiliano na vigezo vya umaskini.
Share this article :
 
Support : Swahiliclan | harold | 0752490120
Copyright © 2011. YOUTH FOR CHANGE - All Rights Reserved
Template Created by swahiliclan Published by hashork
Proudly powered by sc