Dawa ya sangoma yawageukia wanafamilia, wapata kichaa
Mwalimu aliyetumia uchawi kuwaroga wezi, amejikuta akiwaroga shemeji zake waliopata uchizi
Butiama.
Ilikuwa kama simulizi ya kwenye filamu, baada ya mganga wa kienyeji
aliyeletwa toka Kenya kuja kuwaroga wezi walioiba nyumbani kwa Mwalimu
mstaafu, Raphael Omwando (60), baada ya dawa yake kuwatia uchizi ndugu
wa mke mkubwa wa aliyeibiwa.
Mwalimu
Omwando ambaye ana wake wawili alivamiwa na wezi waliomwibia pikipiki
na mali nyingine, ikiwemo kumjeruhi yeye (Omwando) na mkewe mkubwa. Mke
mdogo aliyemuoa hivi karibuni anaishi kwenye nyumba nyingine na
hakuweza kuvamiwa na wezi hao, lakini mke mkubwa alipigwa hadi
kulazimika kupewa matibabu hospitali.
Watu
walio karibu na familia hiyo walisema kutokuelewana kati ya mke mkubwa
na mdogo, kulimfanya mke mkubwa aliyejeruhiwa na majambazi kumtuhumu
mke mdogo kwamba alishirikiana na majambazi hao.
Filamu
hiyo ya familia ilianza kwa ndugu wa mume (Omwando) wanaoishi Kenya,
kuleta sangoma kwa ajili ya kubaini wezi waliomwibia ndugu yao.
“Sijui
nimefikaje hapa hospitali…maana kumbukumbu zinaishia pale
nilipolazimishwa kunywa dawa na mganga wa kienyeji (Sangoma) anayedaiwa
kutokea nchini Kenya …ili wezi wa pikipiki na vifaa vya mwalimu mstaafu
virudishwe,” hiyo ni kauli ya mmoja kati ya watu wanne waliolazwa
hospitali kwa madai ya kurukwa na akili.
Wagonjwa
hao ni vijana wanne wa Kijiji cha Kirumi Kata ya Bukanga, Tarafa ya
Makongoro, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara waliolazwa hospitali ya Mkoa
wa Mara baada ya kunywa dawa hiyo na kupoteza fahamu huku wakionekana
kama mazuzu (Mazombi).
Waathirika
Matiko
Joseph (25) anasema yeye alilazimishwa kunywa dawa nyingi pamoja na
makapi yake,” …Baada ya kumtajia mganga hivyo akasema ninyi kunyweni
nyingi…dawa ilikuwa na ukakasi ilinikereketa sana. Baada ya kunywa
niliondoka lakini baadaye hali ikabadilika sana,” anasema na kuongeza,
“Nilishtukia
niko hospitali tayari ikiwa ni siku ya pili …Nikisimuliwa ilivyokuwa
nazidi kushangaa…huyo mganga alilenga kutuua kabisa….maana wakati
anatoa dawa alisema atakayepata madhara hatapona hata akipelekwa wapi
mpaka vitu virudi ama fedha…akaondoka kwenda Kenya na hakuacha simu
wala jina lake kujulikana,” anasema Joseph huku akipumua kwa
harakaharaka.
Tura
Joseph (30) anasema wengine walikunywa kidogo lakini wao wana ndugu
walilazimishwa kunywa zaidi kwa kile kinachodaiwa kuwa walihisiwa kula
njama za kumdhuru shemeji yao, na ndiyo walidhurika zaidi.
Anasema
baada ya kunywa alihisi kitu kinamkaba shingoni na kuishiwa nguvu,
akawa hoi na kuanza kuongea maneno yaliyowatia shaka, ndugu wakawabeba
kwa bajaji hadi hospitali.