Home » » Sababu Tano(5) za Kutofanikiwa katika Blogging

Sababu Tano(5) za Kutofanikiwa katika Blogging


angry blogger
angry blogger
Katika zama hizi watu wengi sana wanamiliki blogs, za personal, entertainment au matangazo mbali, kila mtu akiwa na dhamira tofauti akilini mwake. Lakini si Kila Blog inayoanzishwa hudumu, wengi hushindwa kufika mbali na hatimaye blogs zao hufa au kukosa wafuatiliaji.
Zifuatazo ni miongoni mwa sababu zinazosababisha Blog nyingi Kutofanikiwa:-
1.Kukosa Content zako Mwenyewe, hatimaye kuanza Ku Copy na Ku Paste
Hili ni jambo ambalo Bloggers wengi wa Hapa kwetu Tanzania Wamelizoea, Ndo maana utakuta habari au makala ileile imeandikwa na Bloggers zaidi ya watano bila kubadilishwa kitu, hii hupunguza taswira ya umakini toka kwa wafuatiliaji wako.

2. Kukosa Ufuatiliaji katika Blogs/Sites zenye Muingiliano na Blog yako.
Kama umedhamiria blog yako iende mbele basi ni jambo la lazima kuwa unatembelea blogs zenye maudhui ya kufanan nawe ili upate changamoto kuhusu nini cha kufanya na kuandika.

3. Kujibu Maswali au Hoja zinazoulizwa sehemu nyingine ambazo hazijapatiwa Ufumbuzi.
Kama ni mtembeleaji wa blogs/sites nyingine unaweza ku observe ni kipi wafutiliaje wanakihoji na hakijapata majibu au maelezo ii wewe ndo iwe sehemu yako ya kujikusanyia wafuatiliaji kwa kuwapa wanachokihitaji.

4. Kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa.
Kama una nia ya dhati ya kufika mbali na Blog yako basi uwe mtu wa kujifunza mara kwa mara toka kwa waliofanikiwa ili nawe utembelea hatua zao katika kukwepa matatizo na kupata mafanikio.

5. Usijiache Peke yako tu, Jichanganye na Bloggers wenzio.
Hii pia ni tatizo kwetu, kwani kuna Bloggers ambao wao wanajiona ndo ma Top, basi hawana muda wa kuwasikiliza hawa wa chini wanaomba nini au ushauri gani wanataka, pia hata kuwawekea link za blogs zao ni shida, pia sisi tunaoanza ku blog tujishirikishe kwa wenzetu ili kukuza traffic na exposure.
Nawasilisha, Tafadhali Toa Maoni yako.
Share this article :
 
Support : Swahiliclan | harold | 0752490120
Copyright © 2011. YOUTH FOR CHANGE - All Rights Reserved
Template Created by swahiliclan Published by hashork
Proudly powered by sc