Katika Articles za nyuma nimeongelea kuhusu umuhimu wa kuwa na Widget hii ambayo husaidia kuongeza Traffic katika Blog yako na pia kufanya Post zako za nyuma kutosahaulika kirahisi.
Njia za Mwanzo zilikuwa ngumu kidogo ila leo nataka niwaeleze kuhusu njia tatu(3) Rahisi mno na hazihitaji mtu kuwa na Utaalam wa Coding kwani Hata Hauhitaji kubadilisha HTML code zako:-
1. Link with In
Hii itakuhitaji kujisajili tu, kisha Utaikuta Widget ya Link With In katika Blog yako na hapo Kila utakapoandika post zako basi zitapata kuonekana na widget hiyo ya Related Post, pia una nafasi ya kuchagua zionekane katika Front Page au Katika Post ndani.
2. N Relate
Hii nayo ni kama Link With In, Ukishajisajili basi unatiririka tu, na utaikuta Widget hiyo Katika LAYOUT ya Blogger Dash Board yako.
3. Out Brain
Hapa napo ni kama katika hizo mbili za juu, yaani ukishajisajili tu na kuandika Blog Address yako basi zinaanza kutokea, muhimu ni kuchagua tu kwamba zitokee juu katika front page au ndani katika Blog Posts.