Vijana walio katika mpango wa Youth for Change Nzega Tabora, wenye
lengo la kuwawezesha kujiajiri kutokana na fursa zilizopo katika Wilaya
ya Nzega, wote wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza
mafunzo ya siku tatu ya ujasiriamali yaliyo fanyika Forest Hotel Nzega.
Mafunzo hayo yalitolewa na mratibu wa shirika la kazi Duniani na
kuratibiwa na taasisi ya Information for Dissemination Network (IDN)
mwezi march 18. 2013.
Picha ya pamoja ya Viongozi wa Youth for Change Nzega Tabora baada ya
mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana, yaliyo funguliwa na Mh. Mkuu wa
Wilaya ya Nzega Bituni Msangi tarehe 18/3/2013 katika Ukumbi wa Forest
Hotel Nzega. Mratibu wa Mafunzo hayo ni Ndugu Boniphace Nyabweta,mwenye
shati la blue bahari wa nne kutoka kulia, wanne kutoka kushoto ni
mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Ndugu. Ngomuo, na Katibu wa CCM Wilaya
mwenye tisheti ya kijani Ndugu Kajoro Vyohoroka ambaye pia alihudhulia
katika siku ya ufunguzi wa mafunzo hayo.