Home » » PATA HABARI MPYA KWENYE BLOG HII

PATA HABARI MPYA KWENYE BLOG HII

Mwalimu akutwa mtupu Shuleni Lindi



 

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha  ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana  na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.
 
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema  walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao  kwa muda na badala yake kwenda kukesha  kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.
Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha  mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule  akiwa uchi wa mnyama.

 http://youthforchang.blogspot.com/



Interpol yamtia mbaroni Alex Massawe Dubai  

 http://youthforchang.blogspot.com/



Alex Massawe 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi 

Posted  Alhamisi,Julai11  2013  saa 9:31 AM
Kwa ufupi
Mkuu wa la Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliliambia gazeti hili jana kwamba Massawe alikamatwa kati ya Juni 20 na 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini.


Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe ambaye alikuwa anatafutwa na Polisi wa Tanzania kwa muda mrefu, amekatwa Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).Mkuu wa la Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliliambia gazeti hili jana kwamba Massawe alikamatwa kati ya Juni 20 na 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini.Babile alisema hivi sasa walikuwa wanaandaa taratibu za kumrudisha nchini ambako amekuwa akisakwa kwa muda mrefu.“Ombi la kuleta mhalifu nchini kutoka nje ya nchi (extradition request), lina hatua ndefu. Unajua kuna mlolongo wa taratibu za kutekeleza ili Massawe aletwe. Kwanza lazima Polisi wa Tanzania watoe tangazo kwa Interpol kuhusu kumsaka mtu huyo ili aletwe,” alisema Babile.Alisema Massawe alikamatwa wakati akifanya taratibu za ukaguzi baada ya kuwasili UAE.Habari zilizofikia gazeti hili mapema kutoka Dubai zilieleza kuwa Massawe alikamatwa na maofisa wa usalama wa UAE kutokana na alama zake za vidole na kuonyesha kuwa alikuwamo kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasakwa na Interpol.
Massawe ambaye anamiliki majumba na biashara ya utalii katika Miji ya Arusha, Dar es Salaam na Moshi, inadaiwa kwamba alikutwa na pasi tatu bandia za kusafiria zilizokuwa na majina tofauti wakati alama zake za vidole zilionyesha anaitwa Alex Massawe.
“Maofisa wa Usalama wa uwanja wa ndege walimuuliza kuwa wewe ndiye Alex Massawe? Alikana lakini alielezwa kuwa alama za vidole vinaonyesha anaitwa hivyo,” kilidokeza chanzo cha habari hizi kwa simu kutoka Dubai. Hata hivyo, Babile alisema hakuwa na taarifa za Massawe kukutwa na pasi bandia za kusafiria.
Uvumi wa Aprili
Mapema Aprili 27, mwaka huu kulikuwa na habari kwamba Massawe amekamatwa katika mji mmojawapo ulioko katika Pwani ya Afrika Kusini.
Habari hizo za kukamatwa kwa Massawe, ambaye pia hufadhili masuala ya kisiasa na michezo, zilisambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya Facebook, Twitter na Jamii Forum. Kulikuwa kuna mkanganyiko wa taarifa huku wengine wakidai alinaswa akiwa ndani ya boti huko Afrika Kusini, wengine wakidai alikamatwa wakati akijaribu kuingia Msumbiji akitokea Malawi.
Akizungumzia hilo Babile alisema huo ulikuwa ni uzushi na baada ya kuzisikia taarifa hizo walifuatilia katika maeneo aliyohusishwa kukamatwa na kubaini kwamba hapakuwa na ukweli wowote.




Share this article :
 
Support : Swahiliclan | harold | 0752490120
Copyright © 2011. YOUTH FOR CHANGE - All Rights Reserved
Template Created by swahiliclan Published by hashork
Proudly powered by sc