Mh. Mkuu wa Wilaya ya Nzega BITUNI MSANGI ameweka mikakati maalumu
ya kuwezesha vijana walio katika mpango wa YOUTH FOR CHANGE kujiajiri kutokana
na fursa za Kilimo na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususani katika
mpango wa miaka mitatu wa Serikali katika kuzalisha ajira Laki sita.
Akizungumza na Viongozi wa Youth
for Change hivi karibuni Ofisini kwake, mara baada ya kurudi kutoka katika
Semina elekezi iliyo andaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda juu ya
usimamizi wa Miradi Sita ambayo ni kipau mbele cha Serikali katika mwaka huu wa
Bajeti 2013/2014, alisema Vijana ni budi wakachangamkia fursa iliyotolewa na
Serikali juu ya Kujikita katika katika Kilimo cha Biashara ili kujikwamua.
Alisema, vijana walio katika
mpango wa kuwezesha vijana kujiajiri maarufu kama
Youth for Change-Nzega, wameonesha mfano mzuri kwa wao kujitambua na kuanza
hivyo Ofisi yake na Halmashauri ya Nzega kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii
watatoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha vijana wanafanikiwa katika mpango
wao wa kujiajiri.
Aidha, alisema hivi sasa kila
kijana asiye na ajira hususani vijana wasomi walio hitimu elimu ya juu, walioko
katika Wilaya yake wanapaswa kujiunga katika mpango huo ili kwa pamoja waweze
kujikita katika kilimo cha biashara sehemu ambayo itazalisha ajira nyingi zaidi
kwa vijana wa mijini na vijijini.
Tayari katika mpango wa vijana
Youth for Change alisha toa eneo kwa ajili ya kilimo katika Kijiji cha Upambo
Kata ya ISANZU Wilayani Nzega lenye heka takribani 700, na vijana tayari
wamejipanga kwa ajiri ya kuanza kilimo cha bustani hivi karibuni wakati
wakisubiri musimu wa kilimo hapo mwezi wa kumi na moja.
Mh. Mkuu wa Wilaya ameweka
mikakati mizuri katika kuhakikisha vijana hao wanafanikiwa ikiwemo mbinu
mbalimbali za kutafuta fedha zitakazo saidia kufanya uwekezaji huwo wa Kilimo.
Kwa upande wa ufugaji wa Nyuki, Bituni Msangi, alisema kuna aja ya kupata
mizinga kwa haraka ili kuweza kuanza kwani ufugaji wa Nyuki ni rahisi na
unafaida kubwa kutokana na asali ya Tabora kupendwa na watu wengi hapa nchini
na nje ya nchi.
Naye Mratibu wa Mpango wa Youth
for Change Ndugu. Boniphace Nyabweta, alisema vijana walio katika mpango wa YFC
wamejipanga vizuri kwani tayari walisha wezeshawa mafunzo ya katika awafu mbili
na taasisi inayo ratibu mpango huo INFORMATION FOR DISSEMINATION NETWORK na
GIVE OPPORTUNITY.
Alisema katika awamu ya kwanza
taasisi zinazo ratibu mpango ziliwawezesha vijana mafunzo juu ya Ujasiriamali,
Afya, Rushwa na Matumizi ya Madawa ya Kulevya yaliyo tolewa na wakufunzi toka
katika Idara mbalimbali za Serikali na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Aidha
katika awamu ya pili vijna waliwezeshwa katika mafunzo ya wiki moja ya
Ujasiriamali ili waweze kuwa na ufahamu juu ya mbinu za kibiashara.