Chadema yaitesa CCM uchaguzi wa udiwani Arusha
- Yaibuka na ushindi wa kishindo katika kata zote nne za Arusha Mjini, wapiga kura wengi washindwa kujitokeza
Arusha.
Chadema kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha
Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye uchaguzi
mdogo wa udiwani uliofanyika jana.
Katika
uchaguzi huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na ambao ulichukuliwa kama
kipimo cha siasa za Arusha ambazo zimekuwa na mvutano mkubwa, Chadema
kiliongoza katikia vituo vyote 136 vya kupigia kura Kata za Elerai,
Kaloleni, Kimandolu na Themi.
Kata
hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua
wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo
(Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni).
Matokeo
Katika
matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Elerai, Obedi
Meng’oriki mshindi alikuwa Jeremiah Mpinga wa Chadema aliyepata kura
2,047 dhidi ya 1,471 za Emmanuel Laizer wa CCM. Katika Kata hiyo
kulikuwa na wagombea wengine ambao ni John Bayo (CUF; kura 302), Seif
Shimba (CCK; kura 3) na Boisafi Shirima (TLP;1).
Katika
Kata ya Themi, Kinabo Edmund wa Chadema aliibuka na ushindi baada ya
kupata kura kupata kura 674. Msimamizi wa Uchaguzi Kata hiyo, Ezeka
Mboya alisema Kinabo alifuatiwa na Victor Mkolwe aliyepata kura 326 na
Lobora Ndarpoi wa CUF alipata kura 307.
Kata
ya Kaloleni, Msimamizi wa Uchaguzi, Anna Ledisa alimtangaza Kessi Lewi
wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 1,470 dhidi ya Emmanuel Mliari wa CCM
aliyepata kura 330 na Abbas Mkindi wa CUF aliyepata kura 275 na
Ngilishi Pauli wa Demokrasia Makini aliyeambulia kura mbili.
Kata
ya Kimandolu, Msimamizi wa Uchaguzi, Suleiman Kilingo alimtangaza
Mchungaji Rayson Ngowi wa Chadema kuwa mshindi kwa kura 2,761 na
kumshinda Edna Saul wa CCM aliyepata kura 1,163. Kwa matokeo hayo,
Chadema sasa kimefikisha madiwani 12 wakati CCM kimebakiwa na kumi na
moja na TLP kina wawili.
Ushindi
huo wa Chadema una athari kwa nafasi ya Meya wa Jiji la Arusha,
Gaudence Lyimo kwani CCM kina wajumbe 14 tu kwenye Baraza la Madiwani,
TLP wawili wakati Chadema sasa kimefikisha 15. Wabunge wa majimbo na
wale wa viti maalumu pia ni madiwani.
Aidha,
Chadema kina nafasi ya kuongeza kiti kingine cha udiwani kwani Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), kinatarajiwa kuitisha uchaguzi mdogo Kata ya
Sombetini.
Mkurugenzi
wa NEC, Julius Malaba alimwambia mwandishi wetu kuwa tume yake
inatarajia kuitisha uchaguzi mdogo hivi karibuni baada ya kata hiyo
kutangazwa wazi na Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tamisemi.
Malaba
alisema uchaguzi huo utaitishwa baada ya aliyekuwa Diwani wake,
Alphonce Mawazo kujitoa CCM na kujiunga na Chadema hali inayokifanya
chama tawala kuwa katika wakati mgumu kukitetea kiti hichoASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU