Wananchi wa Tanzania wameelezwa kuwa kazi ya kuboresha huduma za afya na afya ya mazingira na maji ni ngumu na kuwa inahitaji nguvu za pamoja kati ya jamii, halimashauri na wadau mbalimbali ili kupata mafanikio yaliyokusudiwa hasa ya uzuiaji wa magonjwa.
Akitoa nasaha wakati wa kufunga wa zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa uwiano katika jamii kata ya Gombo la Mboto, Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa, Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema huduma za afya na afya ya mazingira ni muhimu katika maisha ya kila siku ya binadamu.
Ameongeza kwa kuwapongeza sana wakazi wa Gomngo la mboto Markaz pamoja na viongozi wao kwa juhudi kubwa walioifanya katika kuhakikisha uwepo wa kituo cha tiba karibu na jamii na kuwa wanastahili kuwa mfano wa kuigwa na jamii zingine.
Aidha amesema hilo ni moja wapo katika utekelezaji wa agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake la kupeleka huduma za tiba zikiwamo zile za zinazohitaji madaktari bingwa karibu na