Mengi alonga kushamiri kwa dawa za kulevya
“Huwezi kutenganisha rushwa kubwa na dawa za kulevya, hawa wasichana
wetu waliokamatwa Afrika Kusini , lazima kuna mtu mkubwa aliye nyuma
yao,siyo wao,”
Reginald Mengi
Na Boniphace Nyabweta na Protas Charle, Protas Charle
(
email the author)
Posted
Ijumaa,Julai12
2013
Kwa ufupi
- Alisema,
biashara ya dawa za kulevya inayoendelea inatokana na tatizo la utoaji
na upokeaji wa rushwa ambao unaongozwa na watu wakubwa, walioko katika
mfumo halisi wa rushwa.
SHARE THIS STORY
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema, biashara ya
dawa za kulevya inashamiri kutokana na tatizo la rushwa nchini.Mengi
alibainisha hayo jana katika uzinduzi wa ripoti ya mazingira ya
ufanyaji wa biashara nchini 2013, iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF).Alisema,
biashara ya dawa za kulevya inayoendelea inatokana na tatizo la utoaji
na upokeaji wa rushwa ambao unaongozwa na watu wakubwa, walioko katika
mfumo halisi wa rushwa.“Huwezi
kutenganisha rushwa kubwa na dawa za kulevya, hawa wasichana wasanii
wetu, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya na kile kiasi,
lazima kuna mtu mkubwa aliye nyuma yao,siyo wao,” alisema Mengi.Mengi alisema,utashi wa Serikali katika kupambana na rushwa uko kisiasa
ndiyo sababu hakuna utekelezaji na ikiendelea kuwakumbatia na
kuwashikilia mkono watu hao nchi itadondoka.Alisema, taifa linatakiwa kuwatenga watoa rushwa na rushwa zao ili
kuweza kuwa na taifa lenye nguvu kwa kuwa Serikali imeshindwa kupambana
dhidi ya rushwa. kwa kuwa inahofia kukumbwa katika mfumo huo.Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo nchini, Godfrey Simbeye alisema
mazingira ya kufanyia biashara nchini ni magumu kutokana na kodi nyingi
na sheria ngumu zilizowekwa.Simbeye
alisema, utafiti unaonyesha kuwa suala la utozaji wa kodi limekuwa
changamoto kubwa katika biashara kutokana na kuwa na kodi nyingi
zisizoeleweka.“Vikwazo
vikubwa vinavyoyakabili mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini ni
kodi, kumekuwa na kodi nyingi zinazotozwa na zisizoeleweka na sheria
zilizowekwa zinaifanya biashara kuwa ngumu,” alisema.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU.