Home » , » JB APATA DILI LA KIPEKEE AFANYA FILAMU NA WAIGIZAJI WA KUTOKA NORWAY KWENDA KUUZA ULAYA

JB APATA DILI LA KIPEKEE AFANYA FILAMU NA WAIGIZAJI WA KUTOKA NORWAY KWENDA KUUZA ULAYA


Mwigizaji anayependwa sana na mwenye mvuto wa aina yake Jacob Steven a.k.a JB a.k.a Bonge la bwana amepata dili la kufanya filamu na waigizaji wawili maarufu toka nchini Norway Derg na rafiki yake waliokuja nchini mahususi kwa ajili ya kutengeneza filamu hiyo nchini Tanzania.
Akizungumza kwa simu leo mchan na bongomovies.com JB alisema kuwa filamu hiyo imerekodiwa hapa Tanzania ila “final editing” zitafanya huko nchini Norway kabla ya filamu hiyo kutoka rasmi kwenye mwezi wa kumi au kumi na moja.
Filamu hiyo iliyopewa Jina la “Police Lockup” inahusu mwanamke mmoja ambaye alikuwa ameolewa ila hakuwa mwaminifu kwa mume wake na kuanza kutembea na wazungu baada ya hali ya kiuchumi kuwa mbaya.
JB amesema kuwa filamu hiyo ni ya kipekee kwani production yake ni ya uhakika kwani vifaa vilivyotumika kutengenezea filamu hiyo ni vya hali ya juu sana na inatarajiwa kuuzwa nchini nan chi nyingine nyingi duniani kote.
Share this article :
 
Support : Swahiliclan | harold | 0752490120
Copyright © 2011. YOUTH FOR CHANGE - All Rights Reserved
Template Created by swahiliclan Published by hashork
Proudly powered by sc