Home » » Giza nene kidato cha tano

Giza nene kidato cha tano


Giza nene kidato cha tano

Share bookmark Print Email Rating
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Azania, Dar es Salaam wakijisomea katika moja ya darasa la kidato cha tano jana. Picha na Venance Nestory 
Na Fredy Azzah, Mwananchi  (email the author)

Posted  Jumanne,Julai9  2013  saa 8:10 AM
Kwa ufupi
  •  Shule zafunguliwa, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano hawajatangazwa
  •  Baadhi ya shule hatarini kukosa wanafunzi, wamiliki watishia kuzibadili matumizi.
SHARE THIS STORY
0
Share

Matokeo mabaya ya kidato cha nne ya mwaka 2012, yameendelea kuitikisa sekta ya elimu nchini baada ya shule kufunguliwa jana bila kutangazwa kwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu.
Kwa kawaida, wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu, hutangazwa mapema ili kutoa fursa kwa wanafunzi na shule husika kufanya maandalizi ya mahitaji.
Lakini tofauti na ilivyozoeleka, wanafunzi wa kidato cha sita walianza masomo yao jana huku wale wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu wakiwa hawajatangazwa.
Mkanganyiko huo pia unazigusa shule za sekondari za binafsi kwani baadhi zilishachukua wanafunzi wa kidato cha tano na nyingine ziliahirishwa kufunguliwa jana kutokana na kutokuwa na wanafunzi hao.
Hali hiyo imewaacha njia panda baadhi ya wakuu wa shule ambao waliwaambia waandishi wetu kwa nyakati tofauti kwamba wanasubiri maelekezo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu suala hilo, huku wengine wakitishia kufunga shule hizo na kuzigeuza kuwa vyuo vya taaluma nyingine.
Akitangaza matokeo mapya ya kidato cha nne Mei mwaka huu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa aliahidi kwamba majina ya watakaojiunga na kidato cha tano yangetangazwa mapema ili wapate muda wa kujiandaa na kuripoti kwenye shule husika mapema kadri itakavyowezekana.
Jana, Dk Kawambwa hakupatikana kuzungumzia suala hilo na msemaji wa Wizara hiyo, Bunyanzu Ntambi alisema suala la kutangaza majina hayo lipo kwenye ngazi za uamuzi.
“Sababu hasa siwezi kujua, lakini kwa kuwa matokeo yenyewe yalichelewa kutangazwa ni rahisi hata mchakato wa kutangaza waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano uchelewe,” alisema Bunyanzu.
Wakuu wa shule
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Morogoro, Thomas Chihwalo alisema: “Ninachosubiri ni maelekezo ya wizara, nini kifanyike.”
Mkuu wa Sekondari ya Azania, Dar es Salaam, Benard Ngoyaye alipoulizwa alisema: “Nenda kwa Ofisa Elimu wa Wilaya, yeye anafahamu kwa nini majina yamechelewa kufika wakati walikwishachaguliwa.” Mkuu wa Shule ya Sekondari Arusha, Christopher Malamusha alisema walitarajia wizara ingetangaza majina hayo mapema lakini hadi jana walikuwa hawajapokea taarifa zozote.
Mkuu wa Sekondari ya Tambaza aliyejitambulisha kwa jina moja, Zuberi naye alisema wanasubiri maelekezo ya Ofisa Elimu Wilaya ya Ilala.
Share this article :
 
Support : Swahiliclan | harold | 0752490120
Copyright © 2011. YOUTH FOR CHANGE - All Rights Reserved
Template Created by swahiliclan Published by hashork
Proudly powered by sc